Wednesday, November 2, 2011

Mlipuko wa panya

Kumetokea mlipuko wa panya  hapa nchini katika wilaya zipatazo 8 na kuathiri kwa kiasi kukubwa uzalishaji wa mazao shambani na ghalani, kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Mimea katika wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Dkt Fransisca Katagira.
Alizitaji wilaya zilizoathiriwa zaidi na mlipuko huo kuwa ni Bagamoyo na Kisarawe  mkoani Pwani, Nanyumbu mkoa wa Mtwara na Lindi mkoni Mkoani Lindi.
Wilaya nyingine ni zilizopata athari za mlipuko huo wa panya waharibifu ni wilaya ya Morogoro, Kilosa, Mvomero na Ulanga zote za mkoa wa  Morogoro, aliongeza Dkt Katagira.
Alifahamisha kuwa tayari kikosi kazi cha Wizara kimekwenda wilayani Bagamoyo chini ya Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Kuthibiti Balaa la Panya kilichopo Morogoro Vctoria Ngowo ili kupambana na balaa hilo la mlipuko.
Taarifa  za mlipuko wa panya kwa mara ya kwanza zilipokelewa kutoka wilaya ya  Kilosa, kupitia Kituo cha Kuthibiti Balaa la Panya  Agosti 8, 2011, alifafanua Dkt Katagira.
Dkt Katagira ameongeza kuwa panya hao wameshmbulia mbegu shambani zilizopandwa katika msimu wa vuli na kwenye maghala ya kuhifadhi mazao.

No comments:

Post a Comment