Wednesday, November 2, 2011

mkutano wa Kazi kujadili mpango wa uwekezaji katika sekta ya Kilimo

Tanzania inategemea kuwa mwenyeji wa   mkutano wa Kazi kujadili mpango wa uwekezaji katika sekta  ya kilimo kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 10 hadi 11 Novemba mwaka huu, hayo ni kwa mujibu wa Msimamizi wa Misaada  ya Maendeleo na Uratibu wa Mashirikiano wa Kimataifa  katika sekta ya kilimo kutoka  Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika  Margaret Ndaba .
Ndaba amesema zaidi ya wajumbe 200 wanategemea kuhudhuria mkutano huo  kutoka ndani na nje ya nchi  ambao ni wadau wakubwa  wa sekta ya kilimo.
Alizitaja tasisi zitakazoleta wajumbe wake kuwa ni wizara za sekta ya  kilimo hapa nchini, wizara zinazofanyakazi na wizara za sekta za kilimo kama Wizara ya Miundo Mbinu, Fedha,  Ardhi na Mandeleo ya Makazi,  Makamu wa Rais na  Maendeleo ya Jamii,  Wanawake na Watoto.
Wizara nyingine alizitaja kuwa ni wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mawasiliano na Uchukuzi,  Elimu na Ufundi na wizara ya Sayansi na Teknolojia.
Pia wajumbe wa mkutano watatoka Sekta binafsi, Asasi zisizo za kiserikali, Muungano wa vyama vya Ushirika,  Wabia wote waliosaini makubaliano ya kuendeleza sekta ya kilimo hapa Tanzania  ( Tanzania CAADP Compact).
Wadau wakubwa wa kilimo ambao pia ni walengwa   wa mkutano  huu Wakulima,  wataalikwa kupitia  Muungano wa  vikundi  vya Wakulima (MVIWATA).
Tasisi zitakazo kuwa na wajumbe wake kutoka nje ya nchi kuwa ni  pamoja na Umoja wa Africa ( AU), Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa  Mataifa (WFP).

Tasisi nyingine za nje  zitakazoleta wajumbe wake katika mkutano huo  kuwa ni  pamoja na NEPAD,  wawakilishi wa kanda za SADC,  Jumuia ya Afrika mashariki na jumuia ya  COMESA.
Washirika wa Maendeleo  wa  ndani na nje ya nchi pia wamealikwa  katika mkutani huo, ambao aliwataja  kuwa ni Shirika la Misaada Marekani (USAID),  Benki ya Maendeleo ya Afrika  (ADB) na Wawakilishi wa balozi za   nje hapa nchini.
Alisema lengo  kubwa la mkutano  huo ni kujadili mpango mzima wa kuendeleza sekta  za kilimo hapa  nchini  ili kuleta mapinduzi ya kweli katika kilimo kwa  siku za usoni  na hasa  wakati huu wa utekelezaji wa  azma ya Kilimo Kwanza.
Mada zitajikita zaidi kujadili mpango  wa kuendeleza kilimo , utekelezaji wake na gharama husika  ambapo serikali na wadau wake mbali mbali watahitajika kutoa matamko  ya uchangiaji wa mpango huo, aliongeza Ndaba  katika mazungumzo yake.
“Mkutano huo wa siku mbili utafanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar Es Salaam  na  wenyeviti wake watakuwa Mkamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr Gharibu Bilali katika  siku ya kwanza  ya mkutano na siku ya pili ya kikao kitaendeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete “ , alimalizia Ndaba.



No comments:

Post a Comment