Wednesday, January 11, 2012

mkutano wa kuruhusu matumizi ya mbegu mpya ya kilimo

mkutaano wa kuruhusu matumizi ya mbegu mpya unafanyika leo mjini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya New Safari iliyopo mjini hapa
watafiti kutoka katika vituo mbalimbalia vya kilimo hapa nchini wamekutana  na wamekuja na aina mbalimbali za aina za mbegu,
akifungua mkutano huo  kwa niaba ya wazirir wa kilimo chakula na ushirka Bwana Geofrey Kirenga aliwataka wadau wa mkutano huo kuchangagia mada kwa uhakika na umakini zaidi  ili kuruhusu aina hizo mpya za mbegu ambazo ni .

Monday, December 5, 2011

maafisa habari wakutana na kusherrehekea miaka 50 ya uhuru

hapa maafisa habari ambao walimaliza  chuo kikuu cha waislam morogoro 9MUM) mwaka 2008 wakiwa wana adhimisha mika 50 ya uhuru na mika mitatu kazini katika uwanja wa Sabasaba  mjini dsm
hawa ni maafisa habari  sehem nyeti hapa nchini wakiwa wanawajadili baadhi ya mambo

Sunday, December 4, 2011

MIAKA 50 YA UHURU

baadhi ya vyuo vikuu vya Tanzania vilivyosajiliwa kama tulivyolikuta bango katika banda la TCU katika maonesho ya mika 50 ya uhuru yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa JK.Nyerere mjini DSM



Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika (kulia ) Bwana MbogoFutakamba akiwa na Mkurungenzi wa Usalama wa chakula Bwana  emanuel Mtambo

Afisa masoko wa compuni ya uzalishaji wa mbegu ASA Bwana Kawamalakushoto katika banda la wizara ya kilimo chakula na ushirika
Mtaalam wa kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone Bwana Medad akiunganisha mabomba kwa ajili ya umwagiliaji wa mboga

afisa habari wa Rukwa bwana Hamza Temba katika harakati za kumpokea Raisi wa Zanziba  Dr. Shein

Wednesday, November 2, 2011

mkutano wa Kazi kujadili mpango wa uwekezaji katika sekta ya Kilimo

Tanzania inategemea kuwa mwenyeji wa   mkutano wa Kazi kujadili mpango wa uwekezaji katika sekta  ya kilimo kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 10 hadi 11 Novemba mwaka huu, hayo ni kwa mujibu wa Msimamizi wa Misaada  ya Maendeleo na Uratibu wa Mashirikiano wa Kimataifa  katika sekta ya kilimo kutoka  Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika  Margaret Ndaba .
Ndaba amesema zaidi ya wajumbe 200 wanategemea kuhudhuria mkutano huo  kutoka ndani na nje ya nchi  ambao ni wadau wakubwa  wa sekta ya kilimo.
Alizitaja tasisi zitakazoleta wajumbe wake kuwa ni wizara za sekta ya  kilimo hapa nchini, wizara zinazofanyakazi na wizara za sekta za kilimo kama Wizara ya Miundo Mbinu, Fedha,  Ardhi na Mandeleo ya Makazi,  Makamu wa Rais na  Maendeleo ya Jamii,  Wanawake na Watoto.
Wizara nyingine alizitaja kuwa ni wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mawasiliano na Uchukuzi,  Elimu na Ufundi na wizara ya Sayansi na Teknolojia.
Pia wajumbe wa mkutano watatoka Sekta binafsi, Asasi zisizo za kiserikali, Muungano wa vyama vya Ushirika,  Wabia wote waliosaini makubaliano ya kuendeleza sekta ya kilimo hapa Tanzania  ( Tanzania CAADP Compact).
Wadau wakubwa wa kilimo ambao pia ni walengwa   wa mkutano  huu Wakulima,  wataalikwa kupitia  Muungano wa  vikundi  vya Wakulima (MVIWATA).
Tasisi zitakazo kuwa na wajumbe wake kutoka nje ya nchi kuwa ni  pamoja na Umoja wa Africa ( AU), Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa  Mataifa (WFP).

Tasisi nyingine za nje  zitakazoleta wajumbe wake katika mkutano huo  kuwa ni  pamoja na NEPAD,  wawakilishi wa kanda za SADC,  Jumuia ya Afrika mashariki na jumuia ya  COMESA.
Washirika wa Maendeleo  wa  ndani na nje ya nchi pia wamealikwa  katika mkutani huo, ambao aliwataja  kuwa ni Shirika la Misaada Marekani (USAID),  Benki ya Maendeleo ya Afrika  (ADB) na Wawakilishi wa balozi za   nje hapa nchini.
Alisema lengo  kubwa la mkutano  huo ni kujadili mpango mzima wa kuendeleza sekta  za kilimo hapa  nchini  ili kuleta mapinduzi ya kweli katika kilimo kwa  siku za usoni  na hasa  wakati huu wa utekelezaji wa  azma ya Kilimo Kwanza.
Mada zitajikita zaidi kujadili mpango  wa kuendeleza kilimo , utekelezaji wake na gharama husika  ambapo serikali na wadau wake mbali mbali watahitajika kutoa matamko  ya uchangiaji wa mpango huo, aliongeza Ndaba  katika mazungumzo yake.
“Mkutano huo wa siku mbili utafanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar Es Salaam  na  wenyeviti wake watakuwa Mkamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr Gharibu Bilali katika  siku ya kwanza  ya mkutano na siku ya pili ya kikao kitaendeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete “ , alimalizia Ndaba.



Mlipuko wa panya

Kumetokea mlipuko wa panya  hapa nchini katika wilaya zipatazo 8 na kuathiri kwa kiasi kukubwa uzalishaji wa mazao shambani na ghalani, kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Mimea katika wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Dkt Fransisca Katagira.
Alizitaji wilaya zilizoathiriwa zaidi na mlipuko huo kuwa ni Bagamoyo na Kisarawe  mkoani Pwani, Nanyumbu mkoa wa Mtwara na Lindi mkoni Mkoani Lindi.
Wilaya nyingine ni zilizopata athari za mlipuko huo wa panya waharibifu ni wilaya ya Morogoro, Kilosa, Mvomero na Ulanga zote za mkoa wa  Morogoro, aliongeza Dkt Katagira.
Alifahamisha kuwa tayari kikosi kazi cha Wizara kimekwenda wilayani Bagamoyo chini ya Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Kuthibiti Balaa la Panya kilichopo Morogoro Vctoria Ngowo ili kupambana na balaa hilo la mlipuko.
Taarifa  za mlipuko wa panya kwa mara ya kwanza zilipokelewa kutoka wilaya ya  Kilosa, kupitia Kituo cha Kuthibiti Balaa la Panya  Agosti 8, 2011, alifafanua Dkt Katagira.
Dkt Katagira ameongeza kuwa panya hao wameshmbulia mbegu shambani zilizopandwa katika msimu wa vuli na kwenye maghala ya kuhifadhi mazao.