Monday, October 31, 2011


mtambo wa umwagiliaji ujulikanao kama  BIG

sukari mtibwa

huyu ni mtaalam wa umwagiliaji wa kiwanda cha uzalishaji wa sukari cha MTIBWA
kilimo cha umwagiliaji ni kila kitu hapa duniani ,
mitambo ya kuzalisha sukari mtibwa

Wednesday, October 26, 2011

hiki ni chumba cha kudhibiti ufanyaji kazi wa kiwanda cha sukati mtibwa

jithada za kuongeza zao la sukari

shughuli za uzalishaji wa sukari mtibwa
mtaalam wa mashine za umwagilaji katika shamba la mtibwa ikiwa ni jitihada za kuongeza uzalishaji wa sukari

UKIKWEPA YA AL-KAIDA YATAKUPATA YA AL SHABABI

 UKIKWEPA YA  AL-KAIDA YATAKUPATA YA AL SHABABI

Kilichotokea Libya kwa kipindi chote cha miezi minne hadi leo  kiliandaliwa kwa muda usiopungua miaka mnne.  ukiangalia sababu za msingi za kutokea kwa vita ile ilimto Gadafi duniani utagudua ni utajiri wa mafuta ulikuwepo libya
wananchi wa libya walitumia  muda mfupi kuibomoa tripoli  ukilingalnisha na muda uliotumika kuiunda tripoli ya zamani

pesa za walibya zilizokuwa zimewekezwa nje ndio zilizo tumika kuibomoa libya na ndizo zilizotumika kumtoa Gadafi
pamoja na wanalibya kutumia pesa zao na nguvu zao kuijenga libya na kutumia nguvu hizo hizo kuibomoa libya kazi kubwa ipo kwenye kuitengeneza libya mpya ya mwaka 2011 kwa kulipa kodi , hapo ndipo watakapo kubaliana na usemi wa umuhimu wa mkia wa ngo,mbe  unapatika tu pale utakapo katwa

Kwa kipindi chote cha vita vya libya ni afriaka ya kusini tu waliotoa tamko kuhusu vita vya libya ambapo Ris Jacob Zuma alitaka Afrika iachiwe itatue mambo yake yenyewe

mimi naamini kuwa kilichotokea Libya ni matokeo ya utajiri uliokuwepo nchini humo, tusije tukashaanga siku moja tukitangaza kuchimba mafuta yetu yakatukuta ya libya

hata uraniam tulionayo tutakapoanza kuichimba  lolote linaweza kutokea

kwa  sasa botswana sio kwema kuna fukoto kwa sababu ya uchumbaji wa madini kati ya serikali na wanunuzi wa madini

Saturday, October 8, 2011

THAMANI YA ZAO LA KOROSHO IPO KWENYE MABIBO

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika hivi karibuni imekutana na  watafiti kutoka katika  kituo cha utafiti  cha  AMBRAPA kilichopo Brazil ili kufuatilia mradi wa kuongeza thamani ya zao la korosho baada ya kuvunwa Bibi Adelina  Aubert Ng'atigwa alisema kuwa mkutano huo umefanyika baada ya wizara kupeleka wataalam wanne katika kituo hicho nchini brazil kujifunza namna ya kuongeza thamani katika zao la koroshokupitia katika tunda la zao hilo (BIBO)

Aidha wataalam hao walisifia aina nzuri ya korosho inayolimwa nchini na kuwataka wakulima kulitumia tunda la korosho yaani bibo katika kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo juice, keki, pipi  wisk na aina nyingi za mvinyo kama wanavyofanya kule brazili

hata hivyo wizara ipo katika mchakato wa makubaliano na kituo hicho ilikuweza kuwekeza hapa nchini na kuwa wakulima wetu elimu na mbinu mpya za uzalishaji wa zao hilo

CHAKULA KWANZA,... SUKARI BAADAE

Wakati watanzania walio wengi wakitaabika na upatikanaji wa sukari wakulima wa wilaya ya Same wanahofia kukumbwa na njaa kali kama mvua zinazotegemewa kunyesha hazitanyesha
kutokana na mvua kutonyesha kwa muda mrefu  wialyani Same upatikanaji wa chakula umekuwa mgumu kiasi cha watu wengi kushindia uji
akizungumza na kituo cha utangazaji  cha BBC mama mmoja aliyekaririwa kwa jina moja la mama Kangero alisema kuwa watu wengi wanaishi kwa kutegemea kilimo hapa same hivyo kutonyesha kwa mvua ni pigo kwa watu wengi
japo swala la sukari ni muhimu kwa maisha ya kila mtu lakini kwa upande wa Same sera ni moja tu               CHAKULA KWANZA, BAADAE SUKARI

Maadhimisho ya Siku ya Saccos Duniani

maadhidhimisho ya siku ya saccos duniani yatafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia 18,19na 20 katika viwanja vya mashujaa mnazi mmoja hapa Dar es Salaam
kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni saccos hujanga maisha,na katika maadhimisho hayo kutakuwepo na saccos nyingi kutoka ndani  na nje ya Dar es salaam