Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika hivi karibuni imekutana na watafiti kutoka katika kituo cha utafiti cha AMBRAPA kilichopo Brazil ili kufuatilia mradi wa kuongeza thamani ya zao la korosho baada ya kuvunwa Bibi Adelina Aubert Ng'atigwa alisema kuwa mkutano huo umefanyika baada ya wizara kupeleka wataalam wanne katika kituo hicho nchini brazil kujifunza namna ya kuongeza thamani katika zao la koroshokupitia katika tunda la zao hilo (BIBO)
Aidha wataalam hao walisifia aina nzuri ya korosho inayolimwa nchini na kuwataka wakulima kulitumia tunda la korosho yaani bibo katika kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo juice, keki, pipi wisk na aina nyingi za mvinyo kama wanavyofanya kule brazili
hata hivyo wizara ipo katika mchakato wa makubaliano na kituo hicho ilikuweza kuwekeza hapa nchini na kuwa wakulima wetu elimu na mbinu mpya za uzalishaji wa zao hilo
No comments:
Post a Comment