Maonesho ya Wiki ya muhogo yanayotarajia kuanza tarehe 11 mpaka 16 Septemba katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam ambapo uzinduzi utafanyika rasmi tarehe 14 Septemba na mgeni rasmi anategemea kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Uendelezaji wa Mazao, Bwana Beatus Malema alisema maadhimisho hayo yana lengo la kuboresha zao hilo ili liwe zao la chakula na kipato kwa wakulima kuliko wakati huu linapoonekana kuwa ni zao la dharula au la mbadala wakati wa tatizi la njaa.
Zaidi ya taasisi 78 za nje na ndani kushiriki zikiwemo ni pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Tume ya Sayanasi na Teknolojia (COSTECH), World Vision, CONCERN, CRS, CAVA, VECO East Africa, Ofisi za Balozi za hapa nchini, Wakulima, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na nyinginezo.
Kwa mujibu wa Bwana Malema kauli mbiu ya maonesho haya ni “ Muhogo kwa Chakula na Utajiri kwa Wote” .
Bwana Malema ametoa mwito
kwa wadau wa kilimo kuhudhuria kwa wingi katika wiki ya maonesho ya wiki ya muhogo ili kujionea jitihada zinazofanywa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na wadau wake namana wanavyofanya jitihada za kuboresha zao la muhogo kwa lengo la kufikia lengo la milenia la kuondoa umasikini kwa wakulima wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment