Thursday, September 22, 2011

Serikali Yatangaza Mikakati ya kukabili Uhaba wa Sukari

Serikali imechukua hatua madhubuti ili kukabiliana na hali mbaya ya uhaba wa sukari nchini unaosababisha bei kupanda, na kuhakikisha kuwa upungufu wa sukari  kwenye soko la ndani na bei yake inathibitiwa, hayo yalisemwa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Profesa Maghembe, taarifa yake iliyosomwa na Kaimu Katibu Mkuu Geoffrey Kirenga mbele ya nyombo nya habari.

Alisema serikali imeruhusu ununuzi wa tani 120,000 kutoka nje kuingia soko la ndani, sukari hii itafutiwa ushuru wa forodha ili bei yake ilingane na ile ya sukari inayozalishwa ndani ya nchi.

Pia serikali imeamua kufuatilia kwa karibu zaidi uzalishaji na usambazaji wa sukari kutoka viwandani hadi ngazi ya Wilaya, katika kuhakiki kuwa ufuatiliaji unafanikiwa kuanzia sasa kila kiwanda kinatakiwa kuwasilisha serikalini kupitia Bodi ya Sukari,  uzalishaji wake wa kila siku pamoja na taarifa zinazohusu kila mnunuzi, jina la Kampuni namba ya simu ya mkononi ya mwenye kampuni hiyo na  kiasi alichouziwa kwa siku hiyo.

Hatua nyingine ni kufahamu namba za gari yaliyopakia sukari, mwenye gari, wilaya atakayosambaza sukari hiyo na tarehe atakayofika Wilaya husika.

 Makatibu Tawala wa Wilaya zote pia watatakiwa kuleta taarifa hizo wizarani  kila siku kuhusu sukari iliyoingia Wilayani kwao na  kiasi kilichoingi.
Taarifa hiyo pia itatakiwa  kuonyesha sukari imenunuliwa  toka kampuni gani pamoja na vielelezo ikijumuisha namba ya gari na simu ya mwenye gari.

Mkakati mwingine wa serikali wasambazaji wa sukari kutoka viwandani walete Serikalin  kila siku kiasi cha sukari walichopokea kutoka kiwandani pamoja na jina la kiwanda
Ripoti hiyo iataonyesha nani aliuziwa, kampuni na simu ya kiongozi mkuu wa kampuni, kiasi alichouziwa kama ni magunia mangapi ya ujazo au uzito wa kiasi gani, ataisambaza sukari wilaya gani na atafika wilayani lini.
Mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huu au kushindwa kutoa  taarifa sahihi atafutiwa leseni yake mara moja na serikali itachukua hatua za ziada kama itakavyoona inafaa.

No comments:

Post a Comment