Serikali anajipanga kutumia nishati mbadala kama jua na upepo (solar power) katika kuinua na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kama nchi nyingine zilizoendelea. Hayo yalibainishwa na kamatia ya Kilimo ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Eng. Mbogo Futakamba wakati wa ziara yao nchini India ya hivi karibuni .
Aidha Eng. Mbogo amesema, kwa upande wa Tanzania gharama ya nishati ya umeme ni kubwa kuliko uwezo wa wakulima wengi hapa nchini hivyo kushindwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji.
Nishati mbadala kama jua ni muhimu kuwekewa mkazo ili kuwasaidia wakulima kupata nishati ya uhakika kwa ajili ya kutumika katika umwagiliaji vinginevyo itakuwa vigumu kwa Taifa kufikia lengo la kuongeza eneo la umwagiliaji kwa hekta 40,000,000 kwa mwaka huu na lengo la kufikia hekta milioni moja zitakazokuwa zinamwagiliwa ifikapo mwaka 2015.
Sambamba na mikakati ya kukabiliana na tatizo la nishati, Serikali kupitia SAGCOT inampango wa kusimamia kwa ukaribu mipango ya kuwaandaa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa katika kutekeleza shughuli za kilimo chenye tija kinachozingatia uzalishaji usindikaji hadi masoko kwa kutumia fursa ambazo wakulima wakubwa watakuwa nazo.
Aidha Naibu Katibu mkuu amesema Wizara na Kampuni ya Jain Irrigation system Ltd ya nchi hiyo wamekubaliana kuisaidia Tanzania katika kujifunza kwa vitendo na kuzitumia teknolojia zilizoandaliwa na kampuni hiyo katika umwagiliaji na kilimo kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Kamati ya wataalam ya kilimo ilijifunza mbinu mbalimbali za umwagiliaji kwa njia ya matone na kwa njia ya kunyunyizia pamoja na vifaa mbalimbali vinavyohitajika na namna ya kusanifu na kuijenga mifumo hiyo. Pia vifaa mbalimbali vyenye ufanisi katika kusafirisha maji ya umwagiliaji kwenda mashambani ikiwa ni pamoja na mabomba na vile vinavyofaa kwa mifereji ikizingatiwa matumizi kidogo ya maji vilikuwa ni moja ya mafunzo hayo.
Kamati imejifunza teknolojia mbalimbali zinazofaa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya bustani na uzalishaji wa mazao bora kwa kutumia utaalaam wa kiutafiti katika mbegu na vipando mbalimbali ikiwa ni pamoja na mazao ya bustani (tissue culture) pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kusukuma maji kwa ajili ya umwagiliaji zikiambatana na matumizi ya nishati mbadala.
No comments:
Post a Comment