Serikali imeagiza tani 120,000 za sukari kufuatia upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini uliosababishwa na usafirishwaji mkubwa wa sukari nje ya nchi
Aidha mchakato huo utahusisha tani 20,000 ambazo zitaagizwa kutoka katika nchi za SADC katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani na kiasi kingine cha tani 100,000 zitaagizwa kutoka sehemu zinginezo .
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Mohamed Muya alipokuwa anaongea na wandishi wa habari katika ukimbi wa mikutano wa Kilimo I hivi karibuni
Pamoja na hayo serikali imesitisha leseni za kuuza sukari nje ya nchi katika kipindi hiki…. hatua ambazo utekelezaji wake unaanza mara moja.
Katika kuhakikisha kuwa sukari itakayoagizwa inawafikia walengwa , wafanyabiashara wengi watapata lessen za uagizaji wa sukari hiyo kutoka nje ya kupitia taratibu na kanuni za uagizaji wa sukari katika kiwango kisichozidi tani 5000.
Imebainika kuwa upandaji wa bei ya sukari nchini Kenya na Uganda kumepelekea kuadimika kwa sukari nchini kwa kusafirisha nje ya nchi kwa magendo.Bei ya sukari nchini Kenya ni sh4000 kwa kilo na Uganda ni sh3500 kwa kilo.
Kufuatia hali hiyo serikali imechukua hatua kupunguza kasi ya uvushaji wa sukari kinyume na sheria .
Kwa hatua za muda mrefu serikali inaendelea na utekelezaji wa mikakati ya kuongeza uzalishaji wa sukari kwa kiasi kisichopungua tani 550,000.
No comments:
Post a Comment