hapa maafisa habari ambao walimaliza chuo kikuu cha waislam morogoro 9MUM) mwaka 2008 wakiwa wana adhimisha mika 50 ya uhuru na mika mitatu kazini katika uwanja wa Sabasaba mjini dsm
Sunday, December 4, 2011
MIAKA 50 YA UHURU
baadhi ya vyuo vikuu vya Tanzania vilivyosajiliwa kama tulivyolikuta bango katika banda la TCU katika maonesho ya mika 50 ya uhuru yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa JK.Nyerere mjini DSM
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika (kulia ) Bwana MbogoFutakamba akiwa na Mkurungenzi wa Usalama wa chakula Bwana emanuel Mtambo
Wataalam kutoka katika Kituo Cha utafiti cha Kibaha kinachohusika na utafiti wa Muhogo wakiwa wamebeba muhogo katika maonesho ya miaka 50 ya uhuru yaliofanyika katika viwanja vya sabasaba mjini DSM
Afisa masoko wa compuni ya uzalishaji wa mbegu ASA Bwana Kawamalakushoto katika banda la wizara ya kilimo chakula na ushirika
Mtaalam wa kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone Bwana Medad akiunganisha mabomba kwa ajili ya umwagiliaji wa mboga
afisa habari wa Rukwa bwana Hamza Temba katika harakati za kumpokea Raisi wa Zanziba Dr. Shein
Wednesday, November 2, 2011
mkutano wa Kazi kujadili mpango wa uwekezaji katika sekta ya Kilimo
Tanzania inategemea kuwa mwenyeji wa mkutano wa Kazi kujadili mpango wa uwekezaji katika sekta ya kilimo kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 10 hadi 11 Novemba mwaka huu, hayo ni kwa mujibu wa Msimamizi wa Misaada ya Maendeleo na Uratibu wa Mashirikiano wa Kimataifa katika sekta ya kilimo kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Margaret Ndaba .
Ndaba amesema zaidi ya wajumbe 200 wanategemea kuhudhuria mkutano huo kutoka ndani na nje ya nchi ambao ni wadau wakubwa wa sekta ya kilimo.
Alizitaja tasisi zitakazoleta wajumbe wake kuwa ni wizara za sekta ya kilimo hapa nchini, wizara zinazofanyakazi na wizara za sekta za kilimo kama Wizara ya Miundo Mbinu, Fedha, Ardhi na Mandeleo ya Makazi, Makamu wa Rais na Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.
Wizara nyingine alizitaja kuwa ni wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mawasiliano na Uchukuzi, Elimu na Ufundi na wizara ya Sayansi na Teknolojia.
Pia wajumbe wa mkutano watatoka Sekta binafsi, Asasi zisizo za kiserikali, Muungano wa vyama vya Ushirika, Wabia wote waliosaini makubaliano ya kuendeleza sekta ya kilimo hapa Tanzania ( Tanzania CAADP Compact).
Wadau wakubwa wa kilimo ambao pia ni walengwa wa mkutano huu Wakulima, wataalikwa kupitia Muungano wa vikundi vya Wakulima (MVIWATA).
Tasisi zitakazo kuwa na wajumbe wake kutoka nje ya nchi kuwa ni pamoja na Umoja wa Africa ( AU), Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (WFP).
Tasisi nyingine za nje zitakazoleta wajumbe wake katika mkutano huo kuwa ni pamoja na NEPAD, wawakilishi wa kanda za SADC, Jumuia ya Afrika mashariki na jumuia ya COMESA.
Washirika wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi pia wamealikwa katika mkutani huo, ambao aliwataja kuwa ni Shirika la Misaada Marekani (USAID), Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na Wawakilishi wa balozi za nje hapa nchini.
Alisema lengo kubwa la mkutano huo ni kujadili mpango mzima wa kuendeleza sekta za kilimo hapa nchini ili kuleta mapinduzi ya kweli katika kilimo kwa siku za usoni na hasa wakati huu wa utekelezaji wa azma ya Kilimo Kwanza.
Mada zitajikita zaidi kujadili mpango wa kuendeleza kilimo , utekelezaji wake na gharama husika ambapo serikali na wadau wake mbali mbali watahitajika kutoa matamko ya uchangiaji wa mpango huo, aliongeza Ndaba katika mazungumzo yake.
“Mkutano huo wa siku mbili utafanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar Es Salaam na wenyeviti wake watakuwa Mkamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr Gharibu Bilali katika siku ya kwanza ya mkutano na siku ya pili ya kikao kitaendeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete “ , alimalizia Ndaba.
Mlipuko wa panya
Kumetokea mlipuko wa panya hapa nchini katika wilaya zipatazo 8 na kuathiri kwa kiasi kukubwa uzalishaji wa mazao shambani na ghalani, kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Mimea katika wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Dkt Fransisca Katagira.
Alizitaji wilaya zilizoathiriwa zaidi na mlipuko huo kuwa ni Bagamoyo na Kisarawe mkoani Pwani, Nanyumbu mkoa wa Mtwara na Lindi mkoni Mkoani Lindi.
Wilaya nyingine ni zilizopata athari za mlipuko huo wa panya waharibifu ni wilaya ya Morogoro, Kilosa, Mvomero na Ulanga zote za mkoa wa Morogoro, aliongeza Dkt Katagira.
Alifahamisha kuwa tayari kikosi kazi cha Wizara kimekwenda wilayani Bagamoyo chini ya Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Kuthibiti Balaa la Panya kilichopo Morogoro Vctoria Ngowo ili kupambana na balaa hilo la mlipuko.
Taarifa za mlipuko wa panya kwa mara ya kwanza zilipokelewa kutoka wilaya ya Kilosa, kupitia Kituo cha Kuthibiti Balaa la Panya Agosti 8, 2011, alifafanua Dkt Katagira.
Dkt Katagira ameongeza kuwa panya hao wameshmbulia mbegu shambani zilizopandwa katika msimu wa vuli na kwenye maghala ya kuhifadhi mazao.
Monday, October 31, 2011
sukari mtibwa
huyu ni mtaalam wa umwagiliaji wa kiwanda cha uzalishaji wa sukari cha MTIBWA
kilimo cha umwagiliaji ni kila kitu hapa duniani ,
mitambo ya kuzalisha sukari mtibwa
Wednesday, October 26, 2011
jithada za kuongeza zao la sukari
shughuli za uzalishaji wa sukari mtibwa
mtaalam wa mashine za umwagilaji katika shamba la mtibwa ikiwa ni jitihada za kuongeza uzalishaji wa sukari
mtaalam wa mashine za umwagilaji katika shamba la mtibwa ikiwa ni jitihada za kuongeza uzalishaji wa sukari
UKIKWEPA YA AL-KAIDA YATAKUPATA YA AL SHABABI
UKIKWEPA YA AL-KAIDA YATAKUPATA YA AL SHABABI
Kilichotokea Libya kwa kipindi chote cha miezi minne hadi leo kiliandaliwa kwa muda usiopungua miaka mnne. ukiangalia sababu za msingi za kutokea kwa vita ile ilimto Gadafi duniani utagudua ni utajiri wa mafuta ulikuwepo libya
wananchi wa libya walitumia muda mfupi kuibomoa tripoli ukilingalnisha na muda uliotumika kuiunda tripoli ya zamani
pesa za walibya zilizokuwa zimewekezwa nje ndio zilizo tumika kuibomoa libya na ndizo zilizotumika kumtoa Gadafi
pamoja na wanalibya kutumia pesa zao na nguvu zao kuijenga libya na kutumia nguvu hizo hizo kuibomoa libya kazi kubwa ipo kwenye kuitengeneza libya mpya ya mwaka 2011 kwa kulipa kodi , hapo ndipo watakapo kubaliana na usemi wa umuhimu wa mkia wa ngo,mbe unapatika tu pale utakapo katwa
Kwa kipindi chote cha vita vya libya ni afriaka ya kusini tu waliotoa tamko kuhusu vita vya libya ambapo Ris Jacob Zuma alitaka Afrika iachiwe itatue mambo yake yenyewe
mimi naamini kuwa kilichotokea Libya ni matokeo ya utajiri uliokuwepo nchini humo, tusije tukashaanga siku moja tukitangaza kuchimba mafuta yetu yakatukuta ya libya
hata uraniam tulionayo tutakapoanza kuichimba lolote linaweza kutokea
kwa sasa botswana sio kwema kuna fukoto kwa sababu ya uchumbaji wa madini kati ya serikali na wanunuzi wa madini
Kilichotokea Libya kwa kipindi chote cha miezi minne hadi leo kiliandaliwa kwa muda usiopungua miaka mnne. ukiangalia sababu za msingi za kutokea kwa vita ile ilimto Gadafi duniani utagudua ni utajiri wa mafuta ulikuwepo libya
wananchi wa libya walitumia muda mfupi kuibomoa tripoli ukilingalnisha na muda uliotumika kuiunda tripoli ya zamani
pesa za walibya zilizokuwa zimewekezwa nje ndio zilizo tumika kuibomoa libya na ndizo zilizotumika kumtoa Gadafi
pamoja na wanalibya kutumia pesa zao na nguvu zao kuijenga libya na kutumia nguvu hizo hizo kuibomoa libya kazi kubwa ipo kwenye kuitengeneza libya mpya ya mwaka 2011 kwa kulipa kodi , hapo ndipo watakapo kubaliana na usemi wa umuhimu wa mkia wa ngo,mbe unapatika tu pale utakapo katwa
Kwa kipindi chote cha vita vya libya ni afriaka ya kusini tu waliotoa tamko kuhusu vita vya libya ambapo Ris Jacob Zuma alitaka Afrika iachiwe itatue mambo yake yenyewe
mimi naamini kuwa kilichotokea Libya ni matokeo ya utajiri uliokuwepo nchini humo, tusije tukashaanga siku moja tukitangaza kuchimba mafuta yetu yakatukuta ya libya
hata uraniam tulionayo tutakapoanza kuichimba lolote linaweza kutokea
kwa sasa botswana sio kwema kuna fukoto kwa sababu ya uchumbaji wa madini kati ya serikali na wanunuzi wa madini
Saturday, October 8, 2011
THAMANI YA ZAO LA KOROSHO IPO KWENYE MABIBO
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika hivi karibuni imekutana na watafiti kutoka katika kituo cha utafiti cha AMBRAPA kilichopo Brazil ili kufuatilia mradi wa kuongeza thamani ya zao la korosho baada ya kuvunwa Bibi Adelina Aubert Ng'atigwa alisema kuwa mkutano huo umefanyika baada ya wizara kupeleka wataalam wanne katika kituo hicho nchini brazil kujifunza namna ya kuongeza thamani katika zao la koroshokupitia katika tunda la zao hilo (BIBO)
Aidha wataalam hao walisifia aina nzuri ya korosho inayolimwa nchini na kuwataka wakulima kulitumia tunda la korosho yaani bibo katika kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo juice, keki, pipi wisk na aina nyingi za mvinyo kama wanavyofanya kule brazili
hata hivyo wizara ipo katika mchakato wa makubaliano na kituo hicho ilikuweza kuwekeza hapa nchini na kuwa wakulima wetu elimu na mbinu mpya za uzalishaji wa zao hilo
Aidha wataalam hao walisifia aina nzuri ya korosho inayolimwa nchini na kuwataka wakulima kulitumia tunda la korosho yaani bibo katika kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo juice, keki, pipi wisk na aina nyingi za mvinyo kama wanavyofanya kule brazili
hata hivyo wizara ipo katika mchakato wa makubaliano na kituo hicho ilikuweza kuwekeza hapa nchini na kuwa wakulima wetu elimu na mbinu mpya za uzalishaji wa zao hilo
CHAKULA KWANZA,... SUKARI BAADAE
Wakati watanzania walio wengi wakitaabika na upatikanaji wa sukari wakulima wa wilaya ya Same wanahofia kukumbwa na njaa kali kama mvua zinazotegemewa kunyesha hazitanyesha
kutokana na mvua kutonyesha kwa muda mrefu wialyani Same upatikanaji wa chakula umekuwa mgumu kiasi cha watu wengi kushindia uji
akizungumza na kituo cha utangazaji cha BBC mama mmoja aliyekaririwa kwa jina moja la mama Kangero alisema kuwa watu wengi wanaishi kwa kutegemea kilimo hapa same hivyo kutonyesha kwa mvua ni pigo kwa watu wengi
japo swala la sukari ni muhimu kwa maisha ya kila mtu lakini kwa upande wa Same sera ni moja tu CHAKULA KWANZA, BAADAE SUKARI
kutokana na mvua kutonyesha kwa muda mrefu wialyani Same upatikanaji wa chakula umekuwa mgumu kiasi cha watu wengi kushindia uji
akizungumza na kituo cha utangazaji cha BBC mama mmoja aliyekaririwa kwa jina moja la mama Kangero alisema kuwa watu wengi wanaishi kwa kutegemea kilimo hapa same hivyo kutonyesha kwa mvua ni pigo kwa watu wengi
japo swala la sukari ni muhimu kwa maisha ya kila mtu lakini kwa upande wa Same sera ni moja tu CHAKULA KWANZA, BAADAE SUKARI
Maadhimisho ya Siku ya Saccos Duniani
maadhidhimisho ya siku ya saccos duniani yatafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia 18,19na 20 katika viwanja vya mashujaa mnazi mmoja hapa Dar es Salaam
kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni saccos hujanga maisha,na katika maadhimisho hayo kutakuwepo na saccos nyingi kutoka ndani na nje ya Dar es salaam
Thursday, September 22, 2011
Mika 50 ya UHURU na Hali ya Utafiti wa Kilimo
Awamu ya kwanza ya uongozi katika Tanzania iliyo huru ilitimiza jukumu lake la kuleta tija katika sekta ya kilimo kwa kujenga vituo zaidi vya utafiti. Sera na mtazamo katika nyanja ya utafiti ilifanyiwa mabadiliko makubwa kwa lengo la kutatua matatizo ya wakulima wadogo wazalendo, wakulima wa kati na wakulima wenye mashamba makubwa. Vituo kadhaa vilivyoanzishwa kipindi hiki ni KATRIN (1963, mpunga), Uyole (1970, mazao mbalimbali), Hombolo (1972, mtama) na Naliendele (1972, korosho, mbegu za mafuta). Mfumo mzima wa utafiti uliathiriwa na tukio la ghafla la kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Masharika (East African Community, EAC) mnamo mwaka 1977, ambapo kabla ya kuvunjika kwake baadhi ya shughuli za utafiti muhimu kwa nchi wanachama ziliratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Misitu ya Afrika Mashariki (East African Agricultural and Forestry Research Organisation-EAAFRO) iliyokuwa imeanzishwa mwaka 1948 jijini Nairobi. Kituo cha Kibaha kilianzishwa na EAC mwaka 1970 kwa ajili ya kuratibu utafiti wa miwa kwa nchi za Afrika Mashariki.
Mara baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki taasisi ya kitaifa ya utafiti wa kilimo (Tanzania Agricultural Research Organisation, TARO) pamoja na ile ya utafiti wa mifugo (Tanzania Livestock Research Organisation, TALIRO) ziliundwa kwa sheria ya bunge Na….ya mwaka…... Pia, kituo cha Utafiti cha Uyole (Uyole Agricultural Centre, UAC) na kituo cha Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticides Research Institute, TPRI) zilifanywa taasisi zinazojitegemea chini ya wizara yenye dhamana ya Kilimo ambayo iliendelea kuwa mwangalizi mkuu wa shughuli za utafiti katika sekta hiyo. Kabla ya kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki ,TPRI ilikuwa miongoni mwa vituo vya mwanzo kabisa vilivyoanzishwa na Waingereza wakati wa kipindi cha utawala wao. Chini ya muundo huu mpya wa utafiti uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Kwanza, tafiti mbalimbali muhimu katika sekta ya kilimo zilifanyika na kutoa matokeo muhimu yaliyotumika kuongeza uzalishaji. Miongoni mwa matokeo muhimu ya wakati huo ni pamoja na kuzalishwa kwa mbegu mpya za mazao mbalimbali zilizoboreshwa kama zilivyoorodheshwa kwenye Kiamb. Na. 5; sambamba na teknolojia husishi za mbinu bora mbalimbali za ukuzaji wa mazao.
Katika kipindi cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Pili (1985-1990), mabadiliko katika mfumo wa utafiti yalifanyika ambapo TARO na TALIRO (na baadaye UAC) zilivunjwa mwaka 1989 na utafiti ukaanza kusimamiwa moja kwa moja na Wizara yenye dhamana ya kilimo kupitia Idara ya Utafiti na Mafunzo ikiongozwa na kamishna. Idara hii mpya ilijumuisha utafiti wa mazao na mifugo chini ya Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo na iliundwa sambamba na mfumo wa kanda saba za utafiti. Mwaka 2001 utafiti wa mazao na mifugo ulitenganishwa na kila moja ikawa chini ya wizara zenye dhamana ya kilimo au mifugo. Kwa upande wa kilimo, utafiti ukawa chini ya Idara ya Utafiti na Mafunzo ikiongozwa na mkurugenzi (DRT). Mwaka 2007 majukumu ya utafiti na mafunzo yalitenganishwa na kuunda Idara ya Utafiti na Maendeleo chini ya mkurugenzi. Mwaka mmoja baadaye shughuli za utafiti na mafunzo ziliunganishwa tena na kuunda Idara ya Utafiti na Mafunzo chini ya mkurugenzi. Hata hivyo muundo huu haukudumu kwani mwaka mmoja baadaye utafiti na mafunzo vilitenganishwa tena na kuunda idara ya sasa inayoshughulikia utafiti wa kilimo, yaani Idara ya Utafiti na Maendeleo (Division of Research and Development, DRD) ikiongozwa na mkurugenzi chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.
Serikali Yatangaza Mikakati ya kukabili Uhaba wa Sukari
Serikali imechukua hatua madhubuti ili kukabiliana na hali mbaya ya uhaba wa sukari nchini unaosababisha bei kupanda, na kuhakikisha kuwa upungufu wa sukari kwenye soko la ndani na bei yake inathibitiwa, hayo yalisemwa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Profesa Maghembe, taarifa yake iliyosomwa na Kaimu Katibu Mkuu Geoffrey Kirenga mbele ya nyombo nya habari.
Alisema serikali imeruhusu ununuzi wa tani 120,000 kutoka nje kuingia soko la ndani, sukari hii itafutiwa ushuru wa forodha ili bei yake ilingane na ile ya sukari inayozalishwa ndani ya nchi.
Pia serikali imeamua kufuatilia kwa karibu zaidi uzalishaji na usambazaji wa sukari kutoka viwandani hadi ngazi ya Wilaya, katika kuhakiki kuwa ufuatiliaji unafanikiwa kuanzia sasa kila kiwanda kinatakiwa kuwasilisha serikalini kupitia Bodi ya Sukari, uzalishaji wake wa kila siku pamoja na taarifa zinazohusu kila mnunuzi, jina la Kampuni namba ya simu ya mkononi ya mwenye kampuni hiyo na kiasi alichouziwa kwa siku hiyo.
Hatua nyingine ni kufahamu namba za gari yaliyopakia sukari, mwenye gari, wilaya atakayosambaza sukari hiyo na tarehe atakayofika Wilaya husika.
Makatibu Tawala wa Wilaya zote pia watatakiwa kuleta taarifa hizo wizarani kila siku kuhusu sukari iliyoingia Wilayani kwao na kiasi kilichoingi.
Taarifa hiyo pia itatakiwa kuonyesha sukari imenunuliwa toka kampuni gani pamoja na vielelezo ikijumuisha namba ya gari na simu ya mwenye gari.
Mkakati mwingine wa serikali wasambazaji wa sukari kutoka viwandani walete Serikalin kila siku kiasi cha sukari walichopokea kutoka kiwandani pamoja na jina la kiwanda
Ripoti hiyo iataonyesha nani aliuziwa, kampuni na simu ya kiongozi mkuu wa kampuni, kiasi alichouziwa kama ni magunia mangapi ya ujazo au uzito wa kiasi gani, ataisambaza sukari wilaya gani na atafika wilayani lini.
Mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huu au kushindwa kutoa taarifa sahihi atafutiwa leseni yake mara moja na serikali itachukua hatua za ziada kama itakavyoona inafaa.
Wednesday, September 14, 2011
Serikali Haitamvumilia Mfanyabiashara yeyote Atakayesafirisha Sukari kwa Magendo – Waziri Maghembe
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe amekutana na wazalishaji na wasambazaji wa sukari na kuwaagiza kuacha mara moja kusafirisha sukari kwa njia ya magendo na kuiuza nchi za jirani kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi.
Waziri Maghembe alisema si vyema hata kidogo kwa wazalishaji kuzalisha sukari na kisha kuiuza kwa magendo nje ya nchi kwani huo si utaratibu na ni kukiuka sheria na masharti ya leseni walizopewa.
Waziri Maghembe aliwaambia wazalishaji hao kuwa uzoefu aliokuwa nao ni kuwa sukari imepanda kwa kiwango cha juu. Alitoa mfano wa Mkoani Kilimanjaro wiki mbili zilizopita hali ilikuwa mbaya zaidi kwani sukari ilikuwa haipatikani kabisa na kuongeza kuwa matatizo ya kusari kuadimika na inapopatika inauzwa kwa bei ya juu kwa sababu ya wazalishaji na wasambazaji kutokuwa waaminifu kwa Serikali iliyowapa leseni na kuwajengea mazingira mazuri ya wao kuiongoza Sekta ndodo ya Sukari.
Waziri Maghembe alisema wiki hii alifanya ziara katika masoko kadhaa, Jijini Dar es Salaam katika Wilaya ya Temeke, ambapo katika maduka mengi sukari ilikuwa ikiuzwa kwa Shilingi 2,600 kwa Kilo moja na mfuko mmoja wa Kilogramu 50 ulikuwa ukiuzwa kati ya Shilingi 85,000 na Shilingi 105,000.
Waziri Maghembe aliwaambia wazalishaji hao kuwa hali imekuwa hivi kwa sababu Serikali iliamua kwa dhati kulinda soko la ndani na ilifanya hivyo kwa nia nzuri kwa kuwa katika nchi kama Tanzania ambayo sekta binafsi inaendelea kukua ni vyema kulinda viwanda vya ndani na kuonya kuwa kama Wazalishaji hao wakiendelea na hali hii basi Serikali itafikiria utaratibu mwingine.
“Haiwezekani Watanzania wanunue sukari kwa foleni, hii haikubaliki na kamwe Serikali haiwezi kuangalia mambo yakiwa yanaharibika kwa kiwango hiki, ni lazima wazalishaji na wasambazaji muhakikishe Watanzania hawaingii kwenye matatizo” Alikaririwa Waziri Maghembe.
Wazairi Maghembe aliwaambia wazalishaji na wasambazaji hao kuwa Serikali ipo kutekeleza wajibu wake ambao ni kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na mambo mengine kama kutoa vibari vya kuuza sukari kwa utaratibu maalum na si magendo kama ilivyo sasa.
“Tuna ushahidi kuwa sukari iliyo kwenye akiba ya wafanyabiashara ni kidogo kwa kuwa imekuwa ikisafirishwa kwenda nchi jirani kimagendo. Alitoa mfano wa takwimu alizopewa wiki mbili zilizopita zilionyesha kuwa Kilombero Sugar na mfanyabiashara Mohamed Enterprises walikuwa na akiba ya tani 2,300 tu tofauti na uzalishaji ambao huwa ni akiba ya tani 30,000 kwa mwezi na kuongeza kuwa upo ushahidi unaoonyesha kuwa kiwango kikubwa cha sukari inauzwa nje ya nchi.
Akiongea kwa niaba ya Wazalishaji wa Sukari Bwana Ahmad Yahya kutoka Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa alisema sukari imekuwa ikipanda kwa sababu mahitaji ya sukari yamekuwa makubwa na pili wazalishai wamekuwa wakitumia gharama kubwa za uzalishaji. Alizitaja gharama hizo kuwa kupanda kwa bei ya mbolea kutoka Dola 300 mpaka dola 700, bei ya chuma nayo imepanda mara mbili zaidi sambamba na gharama za nishati ya umeme kwa kuwa kumekuwa na tatizo la mgao wa umeme ambalo limechangia gharama ya nishati kupanda mara tatu zaidi ukilinganisha kama wangekuwa wakitumia umeme wa gridi ya taifa.
Waziri Maghembe aliafiki maelezo hayo lakini aliwakumbusha kuwa sababu hizo zilishajadiliwa katika Mkutano alioitisha Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda ambapo baada ya mkutano huo kwa kauli moja wazalishaji walikubali bei ya sukari iuzwe kwa Shilingi 72,000 kwa mfuko wa Kilo 50 bei hiyo ni bila VAT ili na wafanyabisha wanaouza rejareja wakinunua kwa bei hiyo wauze si zaidi ya Shilingi 1,700 kwa Kilo Moja, bei ambayo Watanzania wengi wanaimudu.
Baada ya kusikiliza hoja zao Waziri Maghembe alitoa tamko la Serikali kwa wazalishaji na wasambazaji hao kama ifuatavyo: - Moja Serikali imeruhusu Sukari kiasi cha Tani 100,000 iingizwe mara moja na utaratibu wa vibali utasimamiwa na kuratibiwa na Bodi ya Sukari.
Pili, Lazima Wazalishaji na wasambazaji wauze sukari yao ndani ya nchi ili kumpa unafuu Mtanzania na kama wanataka kuuza sukari nje ya nchi basi waombe vibali vya kufanya hivyo lakini atakayekiuka Serikali itachukua hatua ya kuyakamata magari yanayosafirisha sukari kwenda nchi jirani na kuitaifisha suakari pamoja na magari yalihusika kwenye biashara hiyo ya magendo.
Tatu, Bodi ya Sukari iandae mkutano wa kuwakutanisha Wadau wa sukari kabla ya tarehe 20 Oktoba, 2011.
Nne, Wasambazaji watakaopewa vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi mara watakaponunua sukari hiyo watatakiwa kuonyesha shehema ya sukari waliyoagiza chini ya ukaguzi wa Bodi ya Sukari.
Tano, Serikali inawasiliana na Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania ili kuongeza idadi ya wasambazaji kwa kila Mkoa lakini kwa kuwachagua walio waaminifu tu.
Na mwisho, wazalishaji na wasambazaji kuwa waaminifu kwa kuuza sukari kwa bei elekezi iliyotolewa na serikali yaani Shilingi 72,000 bila VAT kwa mfuko wa Kilogramu 50. Utekelezaji wa maazio hayo unaanza mara moja alisisitiza Waziri Maghembe.
Sunday, September 11, 2011
NISHATI MBADALA KATIKA KUINUA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Serikali anajipanga kutumia nishati mbadala kama jua na upepo (solar power) katika kuinua na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kama nchi nyingine zilizoendelea. Hayo yalibainishwa na kamatia ya Kilimo ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo Eng. Mbogo Futakamba wakati wa ziara yao nchini India ya hivi karibuni .
Aidha Eng. Mbogo amesema, kwa upande wa Tanzania gharama ya nishati ya umeme ni kubwa kuliko uwezo wa wakulima wengi hapa nchini hivyo kushindwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji.
Nishati mbadala kama jua ni muhimu kuwekewa mkazo ili kuwasaidia wakulima kupata nishati ya uhakika kwa ajili ya kutumika katika umwagiliaji vinginevyo itakuwa vigumu kwa Taifa kufikia lengo la kuongeza eneo la umwagiliaji kwa hekta 40,000,000 kwa mwaka huu na lengo la kufikia hekta milioni moja zitakazokuwa zinamwagiliwa ifikapo mwaka 2015.
Sambamba na mikakati ya kukabiliana na tatizo la nishati, Serikali kupitia SAGCOT inampango wa kusimamia kwa ukaribu mipango ya kuwaandaa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa katika kutekeleza shughuli za kilimo chenye tija kinachozingatia uzalishaji usindikaji hadi masoko kwa kutumia fursa ambazo wakulima wakubwa watakuwa nazo.
Aidha Naibu Katibu mkuu amesema Wizara na Kampuni ya Jain Irrigation system Ltd ya nchi hiyo wamekubaliana kuisaidia Tanzania katika kujifunza kwa vitendo na kuzitumia teknolojia zilizoandaliwa na kampuni hiyo katika umwagiliaji na kilimo kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Kamati ya wataalam ya kilimo ilijifunza mbinu mbalimbali za umwagiliaji kwa njia ya matone na kwa njia ya kunyunyizia pamoja na vifaa mbalimbali vinavyohitajika na namna ya kusanifu na kuijenga mifumo hiyo. Pia vifaa mbalimbali vyenye ufanisi katika kusafirisha maji ya umwagiliaji kwenda mashambani ikiwa ni pamoja na mabomba na vile vinavyofaa kwa mifereji ikizingatiwa matumizi kidogo ya maji vilikuwa ni moja ya mafunzo hayo.
Kamati imejifunza teknolojia mbalimbali zinazofaa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya bustani na uzalishaji wa mazao bora kwa kutumia utaalaam wa kiutafiti katika mbegu na vipando mbalimbali ikiwa ni pamoja na mazao ya bustani (tissue culture) pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kusukuma maji kwa ajili ya umwagiliaji zikiambatana na matumizi ya nishati mbadala.
Wednesday, September 7, 2011
umuhimu wa taarifa katika kuinua uchumi wa nchi
Kilimo ni sayansi ambayo mbali na vitendo inahitaji semina za mara kwa mara . moja ya mabo yanayoweza kumbadilisha mkulima ni upatikanaji wa taarifa sahihi kuhusu mabadiliko ya hali ya nchi, matokea ya tafiti mbalimbali pamoja na uhitaji wa soko. kutokana na uhaba wa taarifa katika vijiji vingi wataalam na watafiti mbalimbali kutoka wizara ya kilimo chakula na ushirka wamekuwa wakiwapatia taarifa wakulima na wadau wengine taarifa muhimu kama vichocheo vya mabadiliko ya katika sekta ya kilimo
Tuesday, September 6, 2011
Serikali yajipanga kukabiliana na uhaba wa sukari
Serikali imeagiza tani 120,000 za sukari kufuatia upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini uliosababishwa na usafirishwaji mkubwa wa sukari nje ya nchi
Aidha mchakato huo utahusisha tani 20,000 ambazo zitaagizwa kutoka katika nchi za SADC katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani na kiasi kingine cha tani 100,000 zitaagizwa kutoka sehemu zinginezo .
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Mohamed Muya alipokuwa anaongea na wandishi wa habari katika ukimbi wa mikutano wa Kilimo I hivi karibuni
Pamoja na hayo serikali imesitisha leseni za kuuza sukari nje ya nchi katika kipindi hiki…. hatua ambazo utekelezaji wake unaanza mara moja.
Katika kuhakikisha kuwa sukari itakayoagizwa inawafikia walengwa , wafanyabiashara wengi watapata lessen za uagizaji wa sukari hiyo kutoka nje ya kupitia taratibu na kanuni za uagizaji wa sukari katika kiwango kisichozidi tani 5000.
Imebainika kuwa upandaji wa bei ya sukari nchini Kenya na Uganda kumepelekea kuadimika kwa sukari nchini kwa kusafirisha nje ya nchi kwa magendo.Bei ya sukari nchini Kenya ni sh4000 kwa kilo na Uganda ni sh3500 kwa kilo.
Kufuatia hali hiyo serikali imechukua hatua kupunguza kasi ya uvushaji wa sukari kinyume na sheria .
Kwa hatua za muda mrefu serikali inaendelea na utekelezaji wa mikakati ya kuongeza uzalishaji wa sukari kwa kiasi kisichopungua tani 550,000.
Sunday, September 4, 2011
Maonesho ya Wiki ya muhogo yanakuja….
Maonesho ya Wiki ya muhogo yanayotarajia kuanza tarehe 11 mpaka 16 Septemba katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam ambapo uzinduzi utafanyika rasmi tarehe 14 Septemba na mgeni rasmi anategemea kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Uendelezaji wa Mazao, Bwana Beatus Malema alisema maadhimisho hayo yana lengo la kuboresha zao hilo ili liwe zao la chakula na kipato kwa wakulima kuliko wakati huu linapoonekana kuwa ni zao la dharula au la mbadala wakati wa tatizi la njaa.
Zaidi ya taasisi 78 za nje na ndani kushiriki zikiwemo ni pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Tume ya Sayanasi na Teknolojia (COSTECH), World Vision, CONCERN, CRS, CAVA, VECO East Africa, Ofisi za Balozi za hapa nchini, Wakulima, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na nyinginezo.
Kwa mujibu wa Bwana Malema kauli mbiu ya maonesho haya ni “ Muhogo kwa Chakula na Utajiri kwa Wote” .
Bwana Malema ametoa mwito
kwa wadau wa kilimo kuhudhuria kwa wingi katika wiki ya maonesho ya wiki ya muhogo ili kujionea jitihada zinazofanywa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na wadau wake namana wanavyofanya jitihada za kuboresha zao la muhogo kwa lengo la kufikia lengo la milenia la kuondoa umasikini kwa wakulima wa Tanzania.
Mpunga Kuwa Mkombozi wa Uchumi
Shirika la utafiti na uzalishaji mpunga la Africanrice limeingia mkataba wa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ili kuongeza uzalishaji wa mpunga wa kutosha kwa matumizi ya watazania na baadae kukifanya kilimo hicho kuwa cha kibiashara dunian
Akiongea na wandishi wa habari waziri wa kilimo chakula na Ushirika Mh. Jumanne maghembe amesema shirika hilo kwa kushirikiana na wizara lengo kubwa ni kuhakikisha nchi inazalisha mpunga wa kutosha kwa matumizi ya ndani na kuuza nje na kuifanya Tanzania kuwa nchi moja wapo inayouuza mpunga nchini na nje nchi na kuleta pesa za kigeni
Aidha ushirikiano huo utaanzia katika uzalishaji wa mbegu za mpuga zenye ubora wa hali ya juu na utakao kidhi mahitaji ya soko ili zao hilo kuingia katika soko la dunia kwa alisema Mh.prof Magembe
Katika Sehemu ya pili mheshimiwa waziri alisema itakuwa kufanyia utafiti mbegu za mpunga za aina mbalimbali na kuzifikisha katika vituo vya utafiti baadaye kuwafikie wakulima tayari kwa kuzijaribu ubora wake mashambani
Hata hivyo aliendela kusema kuwa Sehemu ya tatu ilijadiliwekwa na baina ya wizara na Africarice ni kutengenza program ya kuongeza uzalisahaji wa mpunga hapa nchini ambayo itafangeza upatikanaji wa aina mbalimbali ya za mpunga na kufanya chi kupata chakula cha kutosha
Aidha shirika hilo litarajia baada ya mika mitatu litazalisha tani million 27 za mpunga badala ya tani lakin tisa ambazo Tanzania inazalisha kwa mwaka mzima hivi sasa
Program hiyo itaendana na mafunzo ya muda mfupi kwa wataalamu wetu ili kurahisisha kuhamisha teknolijia hiyo kwa wakulima kiurahisi alisema wazira
KILIMO MSETO
hiki ni kilimo mseto ambachi kinachangia kwa kiasi kikubwa urutubishaji wa ardhi ya kilimo....kilimo hakitofautiani na kilimo hifadhi katika upandajia
kilimo hifadhi chenye ni kilimo ambacho hakihitaji kulima au kukatua shamba
Friday, September 2, 2011
MAPINDUZI YA KILIMO YATALETWA NA SERIKALI ZA MITAA
Serikali za mitaa ndio zinazoweza kusababisha mapinduzi ya kilimo kutokea hapa Tanzania
hii inatokana na wao kuwa karibu sana na wakulima na ndio wanaojua tabia halisi ya mkulima
Aidha wapo wakulima wanaoshindwa kufikia malengo sio kwa sababu tu ya kukosa pembejeo za kilimo lakini kukosa uzalendo na kilimo chenyewe
Wapo wakulima wanaolima bila kufuata kanuni za kilimo bora kama vile kuaandaa shamba mapema, kutumia mbegu bora Kupalilia na kuvuna kwa wakati
Wakulima wenye tabia ya namna hii wanapatikana kwa kiasi kikubwa hapa nchini na wenye dhamana ya uhakika kudhibiti hali hiyo ni ERIKALI YA MTAA peke yake, kwa kuzitumia sheria ndogondogo na kuziweka nyingine
Friday, August 26, 2011
mapinduzi ya kijani yanaanzia kwa elimu ya watoto
wanafunzi wakiwa wamebeba jarida la KILIMO USHIRIKA TANZANIA. jarida la wizara ya kilimo ambalo linaelezea utekelezaji mbalimbali wa sera za kilimo Tanzania
Thursday, August 25, 2011
huu ni mhogo kutoka samunge, huu unaweza kustawi sehemu yeyote yenye sifaza kustawisha muhogo
watu wengi hawafahamu kuwa muhongo una faida nyingi kuliko mtu anavyoweza kufikiri
kutokana na mhogo unaweza kupata unga wa ugali, mandazi uji,chips tambi biskuti nasema ukilima mhongo unatakuwa umejiegesha katika kona ya pesa
KILIMO CHAA MAZAO YA BUSTANI HAKIHITAJI MAENEO MAKUBWA
Hili ni kazi vya vijana wajasiriamali wanaojiita MKULIMA MBUNIFU ,kila kiroba kinapandwa miche zaidi ya 20 ukiamua kupata kupitia kilimo unahitaji mtaji kidogo sana
WANAFUNZI MKOANI ARUSHA WAKIJIFUNZA MAMBO MENGI YA KILIMO KWA KUTAMBUA KUWA KILIMO NI SAYANS
kilimo kwanza kinatakiwa kurithishwa kwa watoto ili wabaini kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi .
Na ushirikishwaji wa watoto katika kilimo kutawafanya wasikione kilimo kama ni adhabu na wakione kama kazi nyingine ambazo zinafanywa kwa mashariti ya kazi
TECHNOLOJIA YA UMWAGILIAJI MAJI INAWEZA KUWA MKOMBOZI KWA MKULIMA MDOGO
Mashine hizi za umwagiliajia zinapatikana kwa bei nafuu ambazo mkulima wa kawaida huweza kununua
Hivyo kwa wale wakulima wa mazao ya bustani ni furusa nzuri kwenu
Subscribe to:
Posts (Atom)